MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AKUTANA NA WADAU WA BANDARI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, tarehe 29 Juni 2026 amekutana na Wadau wa Bandari na Taasisi zake kwa lengo la kujadiliana kwa pamoja kuhusu msongamano wa malori ambao kwa kiasi kikubwa umechangiwa na neema ya kuongezeka kwa Shehena ya mzigo katika Bandari ya Dar es Salaam.Amesema Bandari ya Dar es Salaam imekuwa kiufanisi uliopelekea mzigo kuongezeka kufikia tani milioni 30.8 kuelekea mwishoni mwa mwaka wa fedha 2025/2026 ambapo amesema ukuaji huo utakuwa ukiongezeka kila mwaka hivyo hatua za haraka zinatakiwa kuchuliwa kupambana na msongamano wa Malori.Mhe. Chalamila akaongeza kusema kuwa mategemeo ya Bandari ya Dar es Salaam mpaka kufikia 2030 ingefikia lengo hilo lakini limefikiwa kwa mwaka huu wa fedha 2025/2026. Amesema ongezeko la Shehena limepelekea pia ongezeko malori yaliyohudumiwa katika Bandari ya Dar es Salaam ambapo kabla ya uwekezaji idadi ya malori 2100 yalikuwa yanahudumiwa kwa siku na sasa imefikia idadi ya malori 3100 kwa siku baada ya uwekezaji, ikiwa ni ongezeko la malori 1000 kwa siku.
Alitaja sababu nyingine za msongamano wa malori kuwa ni ongezeko la Bandari Kavu Jijini Dar es Salaam, hususani maeneo jirani na Bandari na uwepo wa mizani ya Kurasini.Alibainisha kwamba hatua mbalimbali zimechukuliwa kupambana na changamoto hiyo ikiwa ni pamoja na kuunda timu maalum ili kupata mawazo ya kitaalamu na kuhakikisha sheria na taratibu stahiki zinafuatwa na miundombinu inaboreshwa.Mkuu wa Mkoa amezitaka Taasisi zote ambazo zipo katika mnyororo wa usafirishaji wa mzigo bandarini kukaa meza moja kujadiliana na kuchukua hatua stahiki kwa haraka kutatua changamoto hiyo kwa pamoja.Kikao hiko kimefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Bandari (OSC) ambapo kimehudhuriwa na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Plasduce M. Mbossa

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"