Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, wakati akitoa maelezo kuhusu maboresho yanayofanyika katika Bandari ya Kigoma na Meli Nne za mizigo, zitakazofanya kazi katika Ziwa Tanganyika, wakati wa uzinduzi uliofanyika katika bandari ya Kigoma mkoani Kigoma tarehe 20 Julai, 2026.