Serikali ya Jamhuri ya Rwanda imesema itaendelea kujenga uhusiano mzuri wa kibiashara na Bandari ya Tanga ikiwa ni pamoja na kuendelea kutumia bandari hiyo kupitishia mizigo yao. Hayo yamesemwa na Balozi wa Jamhuri ya Rwanda nchini Tanzania, Mhe. Jenerali Patrick Nyamvumba alipofanya ziara katika bandari hiyo, kwa lengo la kujionea utendaji kazi na kuangalia namna ya kutumia fursa za Bandari ya Tanga.Balozi Nyamvumba amesema kuwa, Bandari ya Tanga imekuwa ni kiunganishi muhimu katika usafirishaji wa mizigo ya kibiashara kutoka na kwenda nchini humo hivyo hakuna budi kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kibiashara. Aidha Balozi Nyamvumba aliipongeza bandari hiyo kwa namna inavyohudumia mizigo ya Rwanda kwa ufanisi mkubwa hali inayopelekea nchi hiyo kuendelea kutumia Bandari ya Tanga.
Awali Kaimu Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Peter Millanzi, akimkaribisha Balozi huyo alisema kuwa, nchi ya Rwanda ni miongoni wa nchi zinazotumia Bandari ya Tanga kupitishia mizigo yao. Miongoni mwa bidhaa za Rwanda zinazopita katika Bandari ya Tanga ni pamoja na Coil, magari, Mitambo mbalimbali na mafuta.Pia Millanzi alisema kuwa Bandari ya Tanga imejipanga katika kuendelea kuboresha utoaji wa huduma kwa wateja wake ili kuwavutia wengi kutumia bandari hiyo.Serikali ya Jamhuri ya Rwanda imesema itaendelea kujenga uhusiano mzuri wa kibiashara na Bandari ya Tanga ikiwa ni pamoja na kuendelea kutumia bandari hiyo kupitishia mizigo yao.