Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dennis Lazaro Londo (Mb) amesema Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ni mdau muhimu katika ustawi wa Viwanda na Biashara nchini.
Mhe.Londo amesema hayo alipotembelea banda la TPA katika Maonesho ya Wakulima yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma.
Amesema Serikali inatambua mchango wa TPA katika ustawi wa Viwanda na Biashara nchini kwa sababu Wafanyabiashara na wamiliki wa Viwanda nchni wanasafirisha bidhaa na malighafi kupitia bandari