Wabunge wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiongozwa na Mhe.Prof. Willy Mishiki Buhini ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Walikale, Kivu Kaskazini, Mei 19,2026 wamekutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed Gallus Abed, ambapo pamoja na mambo mengine wamejadiliana masuala mbalimbali katika kuimarisha ushirikiano na biashara kati ya Tanzania na DRC.Aidha ujumbe huo ulipata fursa ya kutembelea Bandari ya Dar es Salaam kujionea shughuli za utekelezaji bandarini ikiwemo uhudumiaji wa Shehena. Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ni mdau mkubwa wa usafirishaji wa shehena 
kupitia Bandari ya Dar es Salaam ambapo Kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2024 /2025 Bandari ya Dar es Salaam imehudumia mzigo wa Kongo (DRC) tani milioni 5.995 ambayo ni sawa na asilimia 47 ya shehena za Nchi jirani (Transit) zinazohudumiwa na Bandari hiyo ambazo ni Zambia, Uganda, Malawi, Rwanda, Burundi na Zimbabwe.