WADAU WA USAFIRISHAJI WAKUTANA KUIMARISHA BIASHARA YA KIKANDA
Kikao cha siku moja cha Wadau wa Usafirishaji kilichoandaliwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kimefunguliwa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Mjini, Dkt. Rashid Chuachua, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma. Kikao hicho kimewakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji kwa lengo la kujadili fursa na changamoto zinazokabili usafirishaji wa mizigo katika ukanda wa Magharibi. Majadiliano hayo yanalenga kuimarisha biashara ya kikanda na kuongeza ufanisi wa usafirishaji kwa kutafuta suluhu za vikwazo visivyo vya kiforodha, kupunguza ucheleweshaji na gharama za usafirishaji, pamoja na kuimarisha matumizi ya Bandari ya Kigoma kama lango muhimu la biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu na kupitia ushoroba wa kati.

EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"