WAKUU WA TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA WAMETEMBELEABANDA LA TPA KATIKA MAONESHO YA NANE NANE JIJINI DODOMA

Wakuu wa Taasisi mbalimbali za Umma kwa nyakati tofauti wametembelea Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) katika Maonesho ya 32 ya Wakulima (Nanenane) yanayofikia tamati leo katika Viwanja vya Nzuguni jijini Dodoma na kuipongeza Mamlaka kwa ufanisi na mchango wake kwa Taifa kiuchumi.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri Ardhini (LATRA) CPA Habibu J. Suluo ametoa pongezi zake kwa kusema wanatambua na kuthamini mchango wa TPA katika uchumi na kijamii.
Naye Kamishna wa Bima kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Bima Tanzania (TIRA) Dkt. Baghayo Saqware,amesema anatambua mchango wa TPA kwa uchumi wa nchi na umuhimu wa bidhaaa zinazoingia nchini kukatiwa Bima.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Bwa.Salim Msangi ameipongeza TPA kwa ufanisi wa kuhudumia shehena.