Zaidi ya wanafunzi 100 pamoja na Wakufunzi kutoka Chuo cha Bahari Dar es Salaam (DMI), tarehe 23 Juni, 2026 wametembelea Mradi wa Ujenzi wa Matanki ya kuhifadhi na kusambaza mafuta eneo la Vijibweni, Kigamboni Jijini Dar es Salaam, kujifunza kwa vitendo namna Mradi huo unavyotekelezwa. Wanafunzi hao wa Mwaka wa Nne katika Kozi ya Uhandisi katika Mafuta na Gesi walipata maelezo kuhusu Mradi huo wa kimkakati na kujenga uelewa mpana katika masuala mbalimbali kuhusu mradi huo. Maeneo yaliyoangaziwa ni pamoja na Miundombinu ya uhifadhi na usambazaji wa mafuta, Usimamizi na Usalama, Mifumo ya kukabiliana na majanga ya moto pamoja na umuhimu wa Mradi huo katika kukuza uchumi wa nchi na majirani na usimamizi wa uhudumiaji shehena ya mafuta bandarini. Katika ziara hiyo wanafunzi hao wameona kwa vitendo yanayofundishwa darasani