WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA AMETEMBELEA BANDA LA BANDARI YA MTWARA KATIKA MAADHIMISHO YA SIKUKUU YA NANE NANE JIJINI LINDI

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Said Jafo ametembelea Banda la Bandari ya Mtwara katika kilele cha Maadhimisho ya Sikukuu ya Wakulima, Wafugaji na Wavuvi (Nanenane) ambayo yamehitimishwa rasmi tarehe 08 Agosti, 2025 katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi.
Mhe.Dkt. Jafo ameelezea kuvutiwa na utayari wa Bandari ya Mtwara katika kuhudumia shehena mbalimbali ikiwemo mazao ya kilimo kama korosho.
Aidha, ameipongeza Mikoa ya Lindi na Mtwara kwa kufanya maandalizi mazuri ya maonesho hayo ambapo yamekuwa ya mvuto mkubwa kwa Wananchi.