Ujumbe wa Wabunge kutoka Bunge la Jumuiya ya Ulaya umekutana na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika kikao kilicholenga kuangalia namna bora ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na Bandari za Tanzania.

Akizungumza katika kikao hicho kilichofanyika Makao Makuu ya TPA Februari 25,2025 jijini Dar es Salaam,Kiongozi wa Ujumbe huo Mhe.Barry Andrews amesema Ujumbe huo unalengo la kuangalia ni njia zipi nchi zilizo katika Umoja wa Ulaya zinaweza kutumia ili kuendelea kuimarisha uhusiano wa kibiashara na Bandari za Tanzania.

Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw.Plasduce Mbossa ametumia fursa hiyo kuueleza Ujumbe huo mpango wa TPA wa miaka minne kuwa ni kuendelea kuimarisha miundombinu ya kufanyia kazi za kibandari na kuiunganisha Bandari na miundombinu ya reli na barabara ili kurahisisha usafirishaji wa shehena kutoka bandarini.