Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara ameongoza kikao kilichokutanisha ujumbe kutoka Umoja wa Ulaya (UE) na Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kikilenga kuangazia maeneo muafaka ya kushirikiana.

Akifungua Kikao hicho kilichofanyika Julai 3,2025 Makao Makuu ya TPA jijini Dar es Salaam, Prof. Kahyarara ametumia fursa hiyo kuelezea mafanikio ya Serikali katika sekta ya Uchukuzi hususani bandari, ujenzi wa viwanja vya ndege na reli ya mwendokasi (SGR).
Katika salamu zake za ukaribisho Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) Bw.Plasduce Mbossa alielezea kuhusu mradi wa maboresho ya Bandari ya Dar es Salaam (DMGP) na namna ulivyoongeza ufanisi katika uhudumiaji wa shehena.

Kwa upande wake, Mkuu wa Kitengo Uhusiano wa Nchi na Sekta ya Umma Kanda ya Mashariki na Kusini mwa Afika Bw.Christian Elias amesema Umoja wa Ulaya ni mshirika wa miaka mingi wa Tanzania katika Maendeleo akisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kukuza na kuimarisha uchumi.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara amezipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) DP World na Tanzania East Africa Gateway Terminal Limited (TEAGTL) kwa kufanyakazi kwa kushirikiana na kuongeza ufanisi katika kuhudumia shehena.

Katibu Mkuu ametoa pongezi hizo Julai 3,2025 alipotembelea banda la TPA lililopo katika Viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa kwenye viwanja vya Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.


Viongozi na Wananchi kutoka maeneo mbalimbali ya nchi wamejitokeza kwa wingi kutembelea banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani, yanayofikia kilele chake Juni 25,2025, katika Viwanja vya Mnazi mmoja, Kisiwani Unguja, Zanzibar.

Katika maonesho hayo, TPA imetoa Elimu ya ubaharia kwa Wananchi na Wadau mbalimbali ambao wameipongeza Mamlaka kwa ufanisi mkubwa katika kuhudumia shehena kupitia Bandari zake.
Maadhimisho ya Siku ya Mabaharia Duniani yana kauli mbiu isemayo “ Bahari yetu, Wajibu Wetu, Fursa Yetu”.

- NAIBU WAZIRI UCHUKUZI MHE. DAVID KIHENZILE (MB) ATEMBELEA BANDA LA TPA KATIKA MAONESHO YA WIKI YA UTUMISHI WA UMMA DODOMA
- WAKUFUNZI NA WANAFUNZI KUTOKA CHUO CHA MAFUNZO YA ULINZI NCHINI NIGERIA (NISS) WAFANYA ZIARA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
- KATIBU MKUU OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA ATEMBELEA BANDA LA TPA KATIKA MAADHIMISHI YA WIKI YA UTUMISHI DODMA
- TANZIA SALAMU ZA POLE
EN
SW
FR

TPA ChatBot - "Nahodha"