Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) IJP Mstaafu Balozi Ernest Mangu akiwa na Mkurugenzi Mkuu Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania ( TRC) Mha. Machibya Shiwa na Viongozi wengine, Julai 25,2025, wametembelea Bandari Kavu ya Kwala iliyopo Vigwaza, Kibaha Mkoa wa Pwani, kukagua maandalizi ya uzinduzi wake na usafirishaji wa Shehena kwa treni ya SGR kati ya Dar es Salaam na Dodoma, unaotarajiwa kufanywa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wake Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Julai 31,2025.


Bandari ya Dar es Salaam imevuka lengo la utendaji kwa kuhudumia jumla ya Tani Milioni 27.7 kwa mwaka wa fedha 2024/2025 tofauti ya lengo lililowekwa la kuhudumia Tani Milioni 25.
Mafanikio hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed, tarehe 23 Julai 2025 wakati akifungua Kikao cha Tatu (3) cha Baraza la Majadiliano kituo cha Bandari ya Dar es Salaam kilichofanyika mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
“Ninawapongeza sana kwa ufanisi bora kwa mwaka fedha 2024/2025 tumevuka lengo kwa Tani Milioni 2.7 pia tupo mbele ya ufanisi wa jumla ya Tani Milioni 23.69 kwa Mwaka wa fedha 2023/2024, “ alisema Bw. Abed.
Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam amesema mafanikio hayo yametokana na uwekezaji uliofanyika katika Bandari ya Dar es Salaam pamoja ushirikiano wa watendaji wa TPA, wadau mbalimbali na Vyombo vya Usalama waliowezesha shehena kusafirishwa kwa urahisi.
Aidha Bw.Abed amepongeza ushirikiano uliopo kati ya Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari Tanzania (DOWUTA) ambao wamewezesha kudumisha amani na utulivu katika Bandari ya Dar es Salaam.


Maofisa wa Kikosi Maalum cha Kuzuia na Kupambana na Megendo Zanzibar KMKM wakiongozwa na Mkuu wa Utawala na Fedha Capt. Fadhil R. Mberua leo tarehe 21 Julai 2025 wamefanya ziara ya kimafunzo katika Bandari ya Dar es Salaam kujifunza kuhusu usalama wa Bandari , mawasiliano na namna ilivyojidhatiti katika kukabiliana na magendo katika kuhakikisha eneo la bahari linakuwa salama.

Ugeni huo ulipokelewa na Afisa Mwandamizi wa Ulinzi na Usalama katika Bandari ya Dar es Salaam Bw. Fortunatus Sandaria kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed.

- MKUU WA MKOA WA DAR ES SALAAM AFANYA KIKAO NA WADAU KUTOKA SEKTA BINAFSI NA ZA UMMA BANDARI YA DAR ES SALAAM
- MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI TPA ATEMBELEA BANDA LA TPA KATIKA MAONESHO YA SABASABA
- TPA YAIBUKA MSHINDI WA PILI KATIKA TUZO YA MWEZESHAJI WA BIASHARA NA UWEKEZAJI WAKATI WA MAONESHO YA 49 YA KIMATAIFA YA BIASHARA
- TUNAKUTAKIA HERI YA SIKU YA SIKUKUU YA SABASABA
EN
SW
FR

TPA ChatBot - "Nahodha"