Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) leo tarehe 03 Septemba 2025 limefanya kikao cha Thelathini na nane (38) kilichofanyika mjini Morogoro.
Kikao hiko cha siku mbili kimelenga kujadili na kupokea utekelezaji wa bajeti kwa mwaka 2024/2025 na mpango na bajeti kwa mwaka 2025/2026.
Baraza hilo limeongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Mbarikiwa Y. Masinga kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw.Plasduce M. Mbossa.






Msajili wa Hazina, Bw. Nehemia Mchechu, ameipongeza Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kazi nzuri ya kusimamia rasilimali za Serikali kwa ufanisi na weledi.
Bw. Mchechu ametoa pongezi hizo alipofanya ziara ya kikazi katika Bandari ya Tanga, ambapo alikagua shughuli za kiutendaji na kujionea maendeleo ya miradi mbalimbali ya maboresho ya bandari hiyo, inayotekelezwa na Serikali kupitia TPA.
“Bandari ni kiwanda cha pesa cha Serikali. Sehemu kubwa ya mapato ya TRA yanatokana na shughuli za bandari. Ofisi yangu inaiangalia TPA kwa jicho la kipekee kwa sababu mchango wake katika mapato ya taifa ni mkubwa sana,” alisema Bw. Mchechu.
Ameeleza kuwa ofisi yake inafarijika na huduma zinazotolewa katika Bandari ya Tanga, akisisitiza kuwa mafanikio yanayoonekana ni matokeo ya mshikamano na bidii za menejimenti pamoja na watumishi wa TPA.
Aidha, aliwataka wafanyakazi wa TPA kuendelea kuthamini kazi zao na kujivunia utumishi wao ndani ya mamlaka hiyo, akieleza kuwa bandari ni “mboni ya jicho la Serikali.”
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa, amesema mamlaka hiyo itaendelea kutekeleza miradi ya kimkakati kwa niaba ya Serikali ili kuhakikisha Bandari ya Tanga inajengeka kuwa kitovu cha biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Alibainisha kuwa Serikali imewekeza Shilingi bilioni 429.1 katika maboresho ya awali ya bandari hiyo, na tayari uwekezaji huo umeanza kuleta tija kwani mapato yanayokusanywa na TPA kwa kushirikiana na TRA katika kipindi cha miaka miwili yamerudisha gharama hizo.




Kamati ya Maboresho ya Bandari (Port Improvement Committee - PIC) inayojumuisha Wadau wa Sekta ya Uchukuzi kutoka Taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi, imekutana katika kikao chake cha 33 kilichofanyika Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA ) jijini Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti ambaye ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Prof.Godius Kahyarara, ameipongeza TPA kwa kuendelea kuboresha utendaji unachangia kuongeza ufanisi wa sekta nzima ya Uchukuzi nchini, ikiwa ni pamoja na kupunguza msongamano wa malori kuingia na kutoka bandarini na mchakato mzima wa usafirishaji wa shehena.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw Abed Gallus Abed, alisoma taarifa ya utendaji wa Bandari ya Dar es Salaam na kueleza kiwango cha shehena iliyohudumiwa imekuwa ikiongezeka kwa kiwango cha wastani wa asilimia 15 kila mwaka.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) IJP Mstaafu Balozi Ernest Mangu( Picha ya kwanza ameketi katikati suti ya dark blue) na Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa( Picha ya pili) wakiwa katika kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma ( CEOs Forum 2025), kinachofanyika katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha ( AICC).
Kauli mbiu katika Kikao kazi hicho ni “ Ushirikiano endelevu wa Biashara katika Mazingira ya ushindani wa kimataifa, nafasi ya Mashirika ya Umma”.
Mgeni rasmi ni Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) imechukua hatua mbalimbali ikiwemo uboreshaji wa Miundombinu, kusimika mifumo bora ya TEHAMA na kushirikisha Wadau wa Sekta Binafsi wakiwemo waendeshaji wa Bandari, ili kuongeza ufanisi katika kuhudumia Shehena za ndani na nje ya nchi kupitia katika bandari za Mamalaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa wakati akifungua kikao cha Wadau wa Usafirishaji wa Shehena kupitia Ushoroba wa kati, Agosti 21, 2025 Kilichofanyika Wilayani Bagamoyo, Mkoa wa Pwani, Naibu Mkurugenzi Mkuu Mha. Dkt. Baraka Mdima amesema, hatua hizi madhubuti zilichukuliwa na zinaendelea kuchukuliwa na TPA kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuboresha tija Bandarini, ziende sambamba na kujenga utamaduni wa Uadilifu na Uwajibikaji kwa Wafanyakazi wake, wateja na wadau ili kurahisisha ufanyaji biashara kupitia ushoroba wa kati.
Mha. Dkt. Mdima amesisitiza kuwa ni vyema, Wadau wanaoshiriki kikao hicho, wakajadiliana changamoto zinazokabili Sekta ya usafirishaji na kuweka mikakati madhubuti ya kuongeza ufanisi, kupunguza gharama na kurahisisha biashara kupitia ushoroba wa kati.
Aidha, amewahakikishia Wadau wa Usafirishaji kuwa TPA inaendelea kuwa na dhamira ya dhati ya kuendelea kushirikiana na Wadau wake ili kuhakikisha kuwa Ushoroba wa Kati unakuwa wa kisasa, wenye ufanisi, na wenye mchango mkubwa katika maendeleo ya kiuchumi ya Tanzania na nchi zote zinazohudumiwa na ushoroba huo.
Kwa upande wake, Mwakilishi wa Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi Bw. Martin Masunga, amesema maoni yote yaliyotolewa na Wadau hao, yamepokelewa na yatafanyiwa kazi na Serikali ili kurahisisha ufanyaji wa Biashara na kuondoa ucheleweshaji kupitia Ushoroba wa kati.
Kikao hiki cha Wadau wa Usafirishaji kimeandaliwa na TPA chini ya Usimamizi wa Wizara ya Uchukuzi na kimehudhuriwa na Wadau mbalimbali wakiwemo Chama cha Mawakala wa Meli ( TASAA), Chama cha Mawakala wa Forodha ( TACAS) Baraza la Wasafirishaji ( TSC) Wamiliki wa Bandari Kavu ( CIDAT) Chama cha Wasafirishaji Tanzania ( TAT) na Chama cha Wamiliki wa Malori madogo na ya kati ( TAMSTOA)



- WAZIRI MKUU AMEKAGUA MABASI 99 YA MWENDO KASI KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
- KATIBU MKUU PMAESA AMEKUTANA NA MENEJIMENTI YA TPA KATIKA KIKAO KILICHOLENGA KUIMARISHA MAHUSIANO
- WAKUU WA TAASISI MBALIMBALI ZA UMMA WAMETEMBELEABANDA LA TPA KATIKA MAONESHO YA NANE NANE JIJINI DODOMA
- CHUO CHA BANDARI YATOA MAELEZO NA MAFUNZO KWA WANAFUNZI NA WAZAZI KATIKA MAONESHO YA NANE NANE
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"