Maafisa wanafunzi 28 kutoka chuo cha Kijeshi cha Zambia Defence Service Command and Staff College (CSC) wakiongozwa na Kanali Sylvester Kakoma, tarehe 01 Oktoba,2025 wametembelea Makao Makuu ya Mamlaka ya Usimamzi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa ziara ya kujifunza.
Maafisa hao wakisindikizwa na Kanali Robert Mbuba pamoja na Maafisa wengine wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wameishukuru Menejimenti ya TPA kwa mapokezi mazuri na elimu waliyoipata kuhusu shughuli mbalimbali za kibandari, na mchango wake katika biashara na usafirishaji wa kimataifa.
Katika ziara yao hiyo, wamepokelewa na Menejimeni ya TPA ikiongozwa na Mkurugenzi wa Mipango, Ubora na Vihatarishi Dkt. Boniphace Nobeji na Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Dkt. George S. Fasha, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu Bw. Plasduce Mkeli Mbossa.
Meneja wa Bandari ya Tanga Bw.Salehe Mbega, amesema ataendelea kutatua changamoto za wafanyakazi mara tu zinapojitokeza ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi wa hali ya juu na kuleta tija.
Bw. Mbega amesema hayo wakati akifungua kikao cha 69 cha Baraza dogo la Majadiliano (JIC) kwa Bandari ya Tanga, lililofanyika katika ukumbi wa mikutano katika Jengo la Bandari (Bandari House).
Alisema kuwa changamoto hasa za kimaslahi kwa wafanyakazi ni muhimu kupewa kipaumbele, kwani sizipotatuliwa zinaweza kupunguza ari za wafanyakazi katika kutekeleza majukumu yao.
Aidha Bw. Mbega alisisitiza zaidi kwa kusema kuwa, hoja za changamoto nyingine sio lazima zisubiri vikao vya baraza ni vyema kuwasilishwa kwake mapema ili zitatuliwe kwa wakati.
Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyaka wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA) Mkoa wa Tanga, Bw.Aliko Mwakipagala, ametoa pongezi kwa Idara ya Usaidizi wa Biashara kwa kutatua changamoto za wateja haraka pindi zinapojitokeza.
“ Ukweli lazima usemwe idara ya biashara imekua ikitatua changamoto za wateja kwa haraka hasa katika upande wa mifumo inapotokea tatizo wamekuwa msitari wa mbele kuhakikisha tatizo linatatuliwa kwa kweli nawapongeza sana kwa hili “ alisema Bw. Mwakipagala.


Serikali imesisitiza dhamira yake ya kushirikiana na Bandari ya Mtwara ili kuhakikisha mnyororo mzima wa thamani katika usafirishaji wa zao la korosho unatekelezwa kwa ufanisi na mafanikio makubwa.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Mhe. Kanali Patrick Sawala, wakati akifungua Mkutano wa Wadau wa Bandari ya Mtwara, uliofanyika Septemba 29, 2025 mkoani humo, ikiwa ni maandalizi ya msimu wa korosho 2025/2026.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, mwakilishi wake Bw. Emmanuel Mrutu alisema ufanisi wa bandari na utoaji wa huduma bora unategemea kwa kiasi kikubwa ushirikiano wa karibu kati ya bandari na wadau wake.
Kwa upande wake, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Ferdinand Nyathi, alieleza kuwa mkutano huo ni wa umuhimu mkubwa kwani unakutanisha wadau wakuu wanaotumia bandari hiyo, huku ukiwa fursa ya kipekee kwa wateja na wadau kupata mrejesho kuhusu maandalizi ya bandari ya Mtwara katika kuhudumia shehena ya korosho kwa msimu huu wa kilimo.
Aidha, Bw. Nyathi alitumia jukwaa hilo kueleza baadhi ya mafanikio yaliyopatikana katika kuhudumia shehena ya korosho kwenye msimu uliopita, akisisitiza kuwa Bandari ya Mtwara imejipanga vizuri kuhakikisha msimu wa 2025/2026 unakuwa na tija zaidi kwa wakulima na wadau wote wa zao hilo.



Timu ya Mpira wa Wavu ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Bandari Wanawake, imenyakuwa nafasi ya pili katika michuano ya ligi ya Mpira wa Wavu Taifa iliyochezwa katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam.
Bandari Wanawake katika mchezo wake wa fainali imecheza dhidi ya Prisons na kupoteza kwa seti 0-2, matokeo yaliyowaweka TPA kutika nafasi ya pili katika michuano hiyo.
Kwa upande wa Bandari Wanaume, bahati haikuwa upande wao ambapo waliishia katika hatua ya robo fainali katika mchezo uliochezwa Septemba 25, 2025, dhidi ya timu ya Jeshi Stars.
Kwa upande wa Tuzo, Mchezaji Gaudencia Paulo wa Bandari Wanawake ametunikiwa tuzo ya Mzuiaji bora wa mipira ( Best liberal )




- KIKAO CHA KAMATI YA MABORESHO YA BANDARIYA TANGA (PORT IMPROVEMENT COMMITTEE - PIC)
- KIKAO CHA 74 BARAZA LA WAFANYAKAZI LA BANDARI YA DAR ES SALAAM
- MKUU WA MKOA WA TANGA AFANYA ZIARA YA KUKAGUA UTENDAJI KAZI WA BANDARI YA TANGA
- MV GRANDE SHANGHAI IMEWASILI KUTOKA NCHINI CHINA NA KUWEKA HISTORIA KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM
EN
SW
FR


TPA ChatBot - "Nahodha"