Mradi wa ujenzi wa matenki ya kuhifadhi na kusambaza mafuta unaojengwa na Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) umefikia asilimia 33.57 na unatarajiwa kukamilika Agosti, 2026.
Akizungumza wakati alipofanya ziara katika mradi huo, Waziri wa Uchukuzi Mhe.Prof. Makame Mbarawa, amesema mradi huo unaojengwa Kigamboni jijini Dar es Salaam, ni muhimu kwa usalama wa Uchumi wa nchi.
Aidha Mhe.Prof.Mbarawa amesema kukamilika kwa ujenzi wa matenki hayo, kutasaidia kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za kuhudumia meli za mafuta Bandarini.
Katika salamu zake za ukaribisho, Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Mha. Dkt. Baraka Mdima, amesema ujenzi wa matenki hayo umefikia asilimia 33.57 na ukikamilika utapunguza muda wa meli kusubiri kutoka siku 22 mpaka Saba na muda wa kuhudumia meli utapungua kutoka siku Saba mpaka moja.


Serikali imesema maboresho yaliyofanyika katika Bandari zote nchini yameongeza uwezo kuhudumia meli kubwa nakupunguza muda wa meli kusubiri.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Mwigulu Nchemba wakati akifungua Maadhimisho ya Kwanza ya Wiki ya Usafiri Endelevu Ardhini katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yenye kauli mbiu ya Ubunifu na Nishati Safi yanaenda sambamba na Maonesho yanayofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja ambapo banda la TPA limekuwa kivutio kwa Wadau mbalimbali kufika kwa ajili ya kupata elimu ya shughuli za kibandari.
Waziri Mkuu alitoa tuzo kwa Kampuni ya DP World kuonyesha kutambua mchango wake wa udhamini uliofanikisha Maadhimisho hayo.


Wizara ya Uchukuzi imeongoza kikao baina ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya Africa Global Logistics Company (AGL) kutoka Rwanda kilichofanyika Novemba 24,2025 jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika kikao hicho kwa Niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Mkurugenzi wa Miundombinu ya Uchukuzi, Mhandisi Shomari Omari Shomari, amesema kikao hicho kimelenga kufungua fursa za ushirikiano katika sekta ya Uchukuzi na kibiashara kwa ujumla wake.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa AGL Bw. Roger Nkubito amesema dhamira ya kampuni yake ni kuendeleza eneo la Bandari Kavu linalomilikiwa na Serikali ya Rwanda lililopo Isaka ili kuendelea kuimarisha Uchukuzi wa shehena kati ya Bandari za Tanzania na nchi za Rwanda na Burundi.


Wafanyakazi Bandari ya Dar es Salaam waaswa kudumisha utulivu na kuhamasisha amani kwa kuwa Bandari ni sehemu nyeti na pia ni muhimili wa Uchumi katika kuingiza mapato nchini.
Hayo yamesemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed, tarehe 20 Disemba 2025 wakati akufungua Kikao cha kwanza cha Baraza la Wafanyanyakazi Kituo cha Bandari ya Dar es Salaam kilichofanyika mjini Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Amesema kuwa Watumishi wa Umma wanapaswa kuwa wa kwanza Katika kuhamasisha amani nchini hususan katika Bandari ya Dar es Salaam kwa kuwa ni sehemu nyeti hivyo wanatakiwa kujiepusha na mambo ya uvunjifu wa amani huku wakihakikisha wanadumisha utulivu ili kuifanya Bandari kuwa salama, ikiendesha shughuli zake na kuchangia katika kuongeza mapato ya Taifa.
Aidha amekipongeza Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari Tanzania (DOWUTA kwa kuwa kiungo imara katika kuunganisha Menejimenti na Wafanyakazi pamoja na kushirikiana na Menejimenti katika kipindi chote na kuahidi kuendelea kudumisha ushirikiano na DOWUTA pamoja na Wafanyakazi wote.
Pamoja na mambo mengine Baraza hilo limewaaga wajumbe wake ambao wamemaliza muda wao wa utumishi kisheria ambao ni Bi. Hilder Mwakatobe, Bi. Modesta Kaunda, Bw. Mohamedi Telela, Bi. Celina Simon na Bi Brigita Madolomani


Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Salehe Mbega, amesema kuwa, Bandari ya Tanga itaendelea kuweka mazingira rafiki ya utoaji huduma bora ili kuweza kuvutia wateja wengi zaidi kutumia bandari hiyo.
Bw. Mbega amesema hayo wakati wa kikao cha Kamati ya Maboresho ya Bandari ya Tanga (PIC) kinachojumuisha wadau wa bandari hiyo kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano katika Jengo la Bandari (Bandari House).
Amesema kuwa, Bandari ya Tanga itazidi kuboresha huduma zake kwa kuongeza vifaa vya kisasa vya kupakia na kupakua mizigo, kuboresha miundombinu inayotumika kuhifadhi mizigo ya wateja pamoja na kupunguza siku za kuhudumia meli inapokuwa bandarini.
Kwa upande wao wadau wa Bandari ya Tanga wamepongeza juhudi zinazofanywa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania katika kuhakikisha Bandari ya Tanga inatoa huduma bora kwa wateja ikiwemo kuhudumia meli kwa muda mfupi.


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"