Bandari ya Dar es Salaam, terehe 2 Januari 2026 imepokea meli ya kitalii inayoitwa The Crystal Symphony ikiwa na watalii 516 ambao wametembelea vivutio mbalimbali hapa nchini.
Wakala wa Meli hiyo Bw. Gilbert Nikata, amesema meli hiyo ya kifahari inaurefu wa mita 238 kina cha mita 8 imefika Bandari ya Dar es Salaam ikitokea Msumbiji, itakaa kwa siku moja na kuelekea Zanzibar.
Pamoja na mambo mengine ameipongeza Serikali kupitia TPA kwa maboresho makubwa yaliyofanyika katika Bandari hiyo pamoja na huduma bora bandarini hapo na kuahidi ujio wa meli nyingine zaidi za kitalii.
Link: https://www.instagram.com/reel/DS7mMD9iAys/?igsh=bnhpZm4wcXpwa3Fi
Bandari ya Dar es Salaam imeandika historia mpya baada ya kupokea kwa mara ya kwanza meli kubwa ya kisasa inayoendeshwa kwa nishati safi ya gesi asilia (LNG) iitwayo Höegh Australis, inayomilikiwa na kampuni ya Höegh Autoliners kutoka Norway.
Meli hiyo yenye urefu wa mita 200 imeshusha magari 1,006, na inaashiria ongezeko la imani ya makampuni makubwa ya usafirishaji wa kimataifa kwa uwezo wa Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa wakala wa meli hiyo, Bw. Prosper Setebe kutoka kampuni ya EACS (East African Commercial and Shipping Company), ujio wa Höegh Australis ni matokeo ya maboresho makubwa yanayoendelea kufanyika bandarini.
“Bandari ya Dar es Salaam sasa ni lango la kimataifa, si la kikanda tu. Maboresho ya miundombinu, matumizi ya teknolojia na huduma za kisasa vimeivutia meli kubwa kama hii kuleta shehena zake hapa,” alisema Bw. Setebe.
Maboresho hayo ni pamoja na:
• Kuimarika kwa kasi na ufanisi wa kushusha na kupakia mizigo.
• Uwekezaji kwenye vifaa vya kisasa vya kupakua shehena.
• Huduma za kidigitali zinazorahisisha uendeshaji wa shughuli za bandari.
Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imejenga mazingira wezeshi ya kuvutia wawekezaji na kufanya Bandari ya Dar es Salaam kuwa chaguo la kwanza kwa wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi.
“Natoa wito kwa wadau wote kuendelea kuitumia Bandari ya Dar es Salaam kwani sasa ni ya kisasa na ina ufanisi mkubwa,” aliongeza Bw. Setebe.
Ujio wa meli ya LNG ni ishara ya Tanzania kujiweka kwenye ramani ya usafirishaji wa kimataifa kwa kutumia teknolojia rafiki kwa mazingira.
Power, Progress and Port of the Future.
HOEGH AUSTRALIS V5, a cutting edge LNG powered vessel is making its way to Dar es Salaam Port.
Arrival: 29 December 2025
This is more than a ship it’s a symbol of transformation.
DP World is ready. Dar is ready. Tanzania is claiming its place on the global stage.
#DarPort#TPA#DPWorldDar#MaritimeFuture#LNGVessel #TanzaniaRising#GlobalGateway
Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeshiriki kikao cha siku moja cha wadau wa sekta ya usafiri majini kilichofanyika tarehe 29 Desemba, 2025 mkoani Mtwara, kwa lengo la kukusanya maoni ya umma kuhusu mapendekezo ya marejeo ya tozo za huduma za kibandari kwa bandari za mwambao wa Bahari ya Hindi.
Kikao hicho kiliandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na kuongozwa na Meneja wa Udhibiti wa Huduma za Bandari, Bw. Julius Mitinje, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa matakwa ya kisheria kabla ya kupitisha tozo au viwango vipya vya huduma za kibandari.
Akitoa wasilisho katika kikao hicho, mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Josephat Lukindo, amesema mapendekezo haya yana maslahi mapana ya Nchi na lengo lake ni kuboresha ufanisi wa Bandari kwa kuongeza magati, mitambo ya Kisasa ya upakuaji na upakuaji pamoja na maeneo ya kuhifadhia mizigo.
Amefafanua kuwa baadhi ya tozo hizo hazijafanyiwa marekebisho kwa zaidi ya miaka kumi, huku huduma nyingine zikiendelea kutolewa bila kutozwa tozo licha ya kuwa na gharama kubwa za uendeshaji. Aidha, marejeo hayo yanalenga kuziwezesha bandari za Tanzania kutekeleza mipango yake ya uendelezaji wa miundombinu ya bandari, hatua itakayoongeza ufanisi wa utoaji wa huduma na kupunguza gharama katika mnyororo wa usafirishaji kupitia bandari nchini.
Akizungumza kando ya kikao hicho, Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano wa TPA, Dkt. George Fasha, amesema mapendekezo ya marejeo ya tozo yamelenga kuhakikisha bandari za Tanzania zinaendelea kuwa shindani kikanda na kimataifa, zenye ufanisi na zenye uwezo wa kukidhi mahitaji ya sasa na ya baadaye ya biashara ya kimataifa, huku zikichangia kupunguza gharama za usafirishaji, kuongeza ushindani na bandari jirani na kuimarisha uchumi wa Taifa.
Katika kikao hicho, wadau mbalimbali wa sekta ya bandari na usafiri majini wameipongeza TPA kwa kuwasilisha mapendekezo ya tozo yaliyo himilivu na shindani, wakibainisha kuwa mchakato huo umezingatia uwazi, ushirikishwaji wa wadau na maslahi ya pande zote.
Kwa upande wake, TASAC imeeleza kuwa itaendelea kukusanya na kuchambua maoni ya wadau kwa ajili ya kufanya tathmini ya kina kabla ya kutoa mapendekezo ya mwisho kuhusu tozo husika. Maoni ya wadau yataendelea kupokelewa kwa maandishi hadi tarehe 30 Desemba, 2025.



Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeshiriki kikao cha wadau kuhusu kukusanya maoni ya mapendekezo ya marekebisho ya Tozo mbalimbali za huduma za kibandari, kilichoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Kikao hicho cha siku moja kimefanyika tarehe 22 Desemba, 2025, mkoani Tanga, kikiwa na lengo la kuwasilisha maeneo ambayo TPA inapendekeza yafanyiwe marejeo ya tozo za huduma za kibandari, pamoja na kupokea maoni na mapendekezo kutoka kwa wateja na wadau wa sekta ya bandari.
Mchakato huu muhimu ni Kikao cha Kusikiliza Maoni ya Umma, ambapo umma na wadau hupata fursa ya kutoa maoni yao kabla ya kufanyika kwa maamuzi ya mwisho.



- WAZIRI MKUU AFANYA ZIARA KATIKA BANDARI YA LINDI
- WAZIRI MBARAWA ARIDHISHWA NA MAENDELEO YA UJENZI WA BANDARI MPYA YA KISIWA MGAO ILIYOFIKIA ASILIMIA 25
- BARAZA KUU LA MAJADILIANO (CJIC) LA TPA LIMEFANYA KIKAO JIJINI MOROGORO
- MKUU WA WILAYA ARUSHA AFUNGA MKUTANO WA THATHMINI YA UTENDAJI WA SEKTA YA UCHUKUZI
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"