Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Disemba 11 ,2025, imeshiriki kikao cha Wadau kuhusu uthibitishaji wa Tozo za huduma za Kibandari, kilichoandaliwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Kikao hicho cha siku moja kimefanyika Jijini Dar es Salaam, kikiwa na lengo la kukusanya maoni kutoka kwa umma na wadau wa bandari kuhusu mapendekezo ya marekebisho ya tozo za huduma za Kibandari.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Mhe.Adam Malima, amefunga rasmi mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) katika hafla ya utoaji vikombe kwa washindi iliyofanyika katika Uwanja Jamhuri mjini Morogoro Disemba 06,2025.
Katika mashindano hayo TPA imeibuka mabingwa katika michezo ya Netboli,Mpira wa Kikapu (Basketball) na kuvutana kwa Kamba kwa upande wa Wanaume,zote kwa mara ya tano mfululizo.
Kuvutana kwa kamba upande wa wanawake TPA ilishika nafasi ya pili,mbio za kupokezana vijiti wanawake na wanaume nafasi ya pili,huku kwa upande wa mpira wa wavu(wanawake), TPA ilinyakua nafasi ya mshindi wa tatu na Mpira wa kikapu(wanawake) nafasi ya pili.


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imesaini hati ya Makubaliano (MoU) na Kampuni ya Africa Global Logistics (AGL) Tanzania Ltd yenye Makao Makuu yake Nchini Ufaransa ambayo ni kampuni tanzu ya MSC, kwa ajili ya usanifu, Ujenzi na uendeshaji wa gati mpya tatu katika Bandari ya Bagamoyo.
Hati hii ya makubaliano (MoU) imesainiwa tarehe 6 Disemba,2025 Makao Makuu ya TPA Jijini Dar es Salaam kati ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mbossa na Rais wa AGL Philippe Labonne.
Bw. Mbossa amesema, kusainiwa kwa hati ya Makubaliano ni ishara ya utayari wa kuanza kwa mradi wa Bandari mpya ya Bagamoyo ambapo kwa kuanzia AGL itaanza usanifu na Ujenzi wa gati tatu mpya za Kisasa kati ya 28 zinazotatajiwa kujengwa katika Bandari hiyo pamoja na gati mbili mpya za Kisasa katika Bandari ya Dar es Salaam.
Kwa upande wake Rais wa AGL Bw. Philippe Labonne anasema wameamua kuingia makubaliano na TPA na kuwekeza Tanzania kutokana na kuwa nchi yenye Amani, Usalama na mazingira bora na tulivu ya uwekezaji iliyosehemu sahihi kijiografia kwa Sekta ya Uchukuzi na kuwa lango la Biashara Kitaifa na kimataifa.
Mradi wa ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kwa gati mpya tatu utasanifiwa na kujengwa kwa miezi 36 (miaka mitatu) na Kampuni ya AGL imepata nafasi hii ya kushirikiana na TPA katika Ujenzi huo kutokana na uzoefu wao kama kampuni kubwa ya huduma za usafirishaji na logistiki, inayotoa huduma kamili za usafirishaji, usimamizi wa mizigo, usafirishaji wa kimataifa na huduma za forodha, ikiwa sehemu ya kundi la kimataifa la AGL (zamani Bolloré T&L) na sasa wakiwa chini ya MSC.


Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imeibuka mshindi wa kwanza wa tuzo ya umahiri katika uandaaji bora wa hesabu za fedha kwa kuzingatia viwango vya uandaaji hesabu vya kimataifa (IFRS) katika tuzo zilizotolewa na Bodi ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu nchini (NBAA) kwa mwaka wa fedha 2023/2024, zilizofanyika Disemba 4,2025 Jijini Dar es Salaam.
Timu tatu za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) zinazoshiriki mashindano ya Shirikisho la Michezo la Mashirika ya Umma, Taasisi na Makampuni Binafsi nchini (SHIMMUTA) zimefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo yao ya hatua ya robo.
Timu ya Netiboli ilitinga hatua hiyo ya nusu fainali baada ya kuizabua bila huruma timu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) magoli 53 - 32 hiyo ni baada kuwa imeishinda timu Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) jumla ya magoli 57 - 20 katika mchezo wa 16 bora.
Timu mbili za mchezo wa kuvutana kwa kamba (wanaume na wanawake) nazo zimetinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda michezo yao ya robo fainali dhidi ya MUHAS kwa wanaume na dhidi ya MNH kwa wanawake, huku timu ya Mpira wa kikapu ikitinga hatua ya robo fainali kwa kuizaba timu ya Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania TFRA) jumla ya vikapu 52 - 18 na sasa itacheza nusu fainali na timu ya TFS.
Timu za Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ambao ndio mabingwa wa jumla wa michuano iliyopita zimeendelea kufanya vizuri kwa kufanikiwa kuingia hatua ya robo fainali ambazo ni Mpira wa wavu (Volleyball ke na me) ,Mpira wa kikapu (wanawake)


EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"