Bandari ya Kilwa imeendelea kuwa nguzo kubwa ya kuvutia, kukuza na kuendeleza Sekta ya Utalii Nchini kufuatia kuwasili kwa Meli ya MV LE BELLOT, tarehe 11 Februari, 2026 ikiwa na jumla ya watalii 152 pamoja na wafanyakazi 133.
Ujio wa Meli hiyo unawapa Watalii hao fursa ya kutembelea na kujionea urithi wa kipekee pamoja na vivutio vya kihistoria na kitamaduni vilivyopo Kilwa Kisiwani, eneo lenye umuhimu mkubwa kihistoria.
Watalii hao wanatoka katika Mataifa mbalimbali Duniani ikiwemo Kenya, Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa, Canada, Australia, Uswisi, Hispania, Shelisheli, Norway, Chile na Ubelgiji.
Mchanganyiko huo wa Mataifa unaendelea kuthibitisha hadhi ya Tanzania kama kitovu cha utalii kinachozidi kuvutia Kimataifa. Mafanikio haya yanatokana na juhudi za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha na kuboresha Sera, Sheria, Miundombinu, Kuendeleza maeneo ya urithi na Kutangaza vivutio vya Utalii nje ya Nchi.
Aidha, juhudi kubwa zimeendelea kutekelezwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania katika kuboresha huduma na mazingira ya upokeaji wa meli mbalimbali ikiwemo za Utalii, hatua inayochochea hamasa kwa wadau wa sekta hiyo na kufanya Bandari za Tanzania kuwa chaguo la kuaminika.
Ongezeko la ujio wa Meli za Utalii ni ishara ya mafanikio ya mikakati ya Kitaifa ya kukuza Utalii, Kuongeza mapato ya Nchi, kufungua milango ya fursa za ajira na biashara kwa wananchi wa maeneo husika. Tanzania inaendelea kusonga mbele na kuwa kivutio bora cha Utalii Barani Afrika na Duniani kwa ujumla.
Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na wafanyakazi wote wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), wanakupongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kutimiza siku 100 madarakani tokea kuapishwa.
Serikali imesema uwekezaji wa zaidi ya Shilingi bilioni 590 unaoendelea kufanyika katika Bandari ya Mtwara na Bandari mpya ya Kisiwa Mgao unalenga kufungua na kuimarisha ushoroba wa Kusini, hatua itakayochochea ukuaji wa biashara na uchumi katika ukanda huo pamoja na nchi jirani.
Kauli hiyo imetolewa Februari 11, 2026 na Naibu Waziri wa Uchukuzi, Mhe. David Kihenzile (Mb), alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa mradi wa Bandari mpya ya Kisiwa Mgao pamoja na maboresho yanayoendelea katika Bandari ya Mtwara.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Kihenzile amesema Serikali ya Awamu ya Sita imeendelea kuwekeza kimkakati katika miundombinu ya bandari ili kuongeza ufanisi wa huduma, kupunguza gharama za usafirishaji na kuvutia wawekezaji zaidi katika sekta za viwanda, kilimo na madini. Ameeleza kuwa maboresho hayo yataifanya Bandari ya Mtwara na Kisiwa Mgao kuwa lango muhimu la biashara kwa mikoa ya Kusini na nchi za SADC.
Aidha, ameonesha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa mradi huo na kusisitiza umuhimu wa kuzingatia ubora, muda wa utekelezaji na thamani ya fedha katika kukamilisha kazi hiyo.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma za Uhandisi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), Mha.Erick Madinda, akimwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TPA Bw. Plasduce Mkeli Mbossa, amesema mradi wa ujenzi wa Bandari ya Kisiwa Mgao umefikia asilimia 33 ya utekelezaji wake na unaendelea vizuri kulingana na ratiba iliyopangwa.
Mha. Madinda ameongeza kuwa kukamilika kwa mradi huo kutapanua uwezo wa kuhudumia shehena kubwa zaidi ya mzigo mchafu na malighafi zake, hivyo kuifanya Bandari ya Mtwara na Kisiwa Mgao kuwa kitovu cha biashara katika ukanda wa Kusini mwa Tanzania.
Mradi huo unatarajiwa kukamilika kwa wakati na kwa viwango vilivyokusudiwa, huku ukiwa sehemu ya mkakati mpana wa Serikali wa kuboresha sekta ya uchukuzi na kuimarisha uchumi wa taifa kupitia miundombinu ya kisasa ya Bandari.


Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Salehe Mbega amewapongeza wafanyakazi wa Bandari hiyo kwa kuchapa kazi kwa bidii na kuiwezesha kupata mafanikio makubwa.
Bw. Mbega ametoa pongezi hizo wakati wa kikao cha 39 cha Baraza la Wafanyakazi Bandari ya Tanga kilichofanyika bandarini hapo.
Katika kikao hicho, Baraza lilipokea taarifa ya utendaji kazi wa Bandari ya Tanga kwa kipindi cha miezi sita ya Julai hadi Disemba 2025. Pia Baraza hilo lilijadili mapendekezo ya malengo na bajeti mpya ya Bandari kwa mwaka wa fedha 2026/ 2027.
Aidha Baraza hilo lilikubaliana kuendelea kufanya kazi ufanisi mkubwa ili kupata tija kubwa zaidi katika kuhudumia wateja wanaopitishia mizigo yao katika Bandari ya Tanga.
Aidha katika hatua nyingine, Bw. Mbega amewashukuru wajumbe wa baraza hilo kwa mchango wao ulioiwezesha Bandari ya Tanga kupata mafanikio makubwa.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Ajira na Mahusiano, Mhe. Deus Sangu (Mb), ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa uwasilishaji bora wa michango na utoaji wa huduma kwa wanachama wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Mhe. Sangu ametoa pongezi hizo Februari 09, 2026, wakati wa uzinduzi wa Sera ya Taifa ya Kinga ya Jamii uliofanyika katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC), jijini Arusha, ambapo alikabidhi cheti cha pongezi kwa TPA. Cheti hicho kilipokelewa na Afisa Rasilimali Watu Mkuu wa TPA, Bi. Edna Kitila.
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"