Katika kuhakikisha Kauli Mbiu ya maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja kwa mwaka 2025 “Mission Possible” inatekelezwa kwa vitendo, Bandari ya Tanga imejipanga kuilinda mizigo ya wateja ili iweze kutoka bandarini ikiwa salama.
Uhakikisho huo umetolewa na Afisa Ulinzi Mwandamizi wa Bandari ya Tanga Bw. Rajani Fidu Hussein katika mwendelezo wa wiki ya Huduma kwa Wateja alipokuwa anawahudumia huduma maeneo katika yake ya kazi.
Bw. Fidu alisema kuwa Bandari ya Tanga ni salama ulinzi wa mizigo ni wa uhakika, hivyo nawashauri wateja waendelee kutumia Bandari ya Tanga ambayo iko tayari kutoa huduma na kutatua changamoto za wateja usiku na mchana.


Bandari ya Mtwara imeanza rasmi kupokea na kuhudumia meli zenye shehena za mafuta yanayosafirishwa kwenda Nchi jirani za Zambia na Malawi ikiwa ni hatua muhimu katika kuimarisha biashara na usafirishaji wa bidhaa.
Akiongea Oktoba 08,2025 wakati wa hafla ya mwendelezo wa maadhimisho ya Wiki ya Huduma kwa Wateja, Meneja wa Bandari ya Mtwara, Bw. Ferdinand Nyathi amesema, huduma hiyo imeanza kutolewa tangu mwezi Septemba na kuendelea mwezi huu wa Oktoba ambapo ujio wa meli hizo ni ishara ya maendeleo makubwa katika Bandari ya Mtwara kwa kuwa awali haikuhudumia shehena za mafuta kwa ajili ya nchi hizo jirani.
Ameongeza kuwa, kasi ya usafirishaji wa mizigo kupitia Bandari ya Mtwara imeongezeka kwa kiwango kikubwa ambapo kwa sasa inahudumia zaidi ya tani milioni 2.5 kwa mwaka 2024/2025 ikilinganishwa na tani 500,000 kwa mwaka 2021/2022.
Kwa upande wa baadhi ya wadau wa Bandari walioshiriki hafla hiyo, wamepongeza maboresho yaliyofanyika kwenye miundombinu na vifaa ambapo huduma zimeimarika kwa kiwango kikubwa. Wamepongeza pia uongozi wa Bandari kwa kuendelea kushirikiana na wadau katika kuboresha huduma.


Bandari ya Tanga mevunja rekodi katika kuhudumia meli, shehena na ukusanyaji wa mapato katika kipindi cha robo mwaka cha Julai - Septemba 2025.
Hayo yamesemwa na Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Salehe Mbega wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Huduma Kwa Wateja ambayo uadhimishwa Mwezi Oktoba ya kila Mwaka.
Mbega amesema katika kipindi cha robo mwaka Julai - Septemba 2025 Bandari ya Tanga imehudumia meli 52 za bahari ya mbali (deep sea) wakati lengo lilikuwa kuhudumia meli 37 sawa na ongezeko la asilimia 40.5.
Aidha, idadi ya hiyo ya meli zilizohudumiwa kwa kipindi hicho ni zaidi kwa asilimia 30 au meli 12 ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha Julai - Septemba 2024 ambapo idadi ya meli zilizohudumiwa zilikua 40
Pia Meneja huyo amesema kwa upande wa shehena ya mzigo kwa kipindi cha Julai - Septemba 2025 bandari imehudumia tani 508,373 wakati lengo lilikuwa kuhudumia tani 413,591 sawa na ongezeko la asilimia 22.9 ya lengo.
Aidha kiasi hicho cha shehena kilichohudumiwa kilikua ni zaidi kwa tani 174,730 au asilimia 52.37 kikilinganishwa na kipindi kama hicho cha Julai - Septemba 2024 ambapo bandari ilihudumia tani 333,643.
Halikadhalika, kwa upande wa mapato Mbega amesema katika kipindi cha Julai - Septemba 2025 Bandari ya Tanga imekusanya jumla ya Shilingi
Bilioni 31.671 wakati lengo lilikuwa ni kukusanya Shilingi Bilioni 21.350 sawa na ongezeko la asilimia 48.34.
Vievile, kiasi hicho cha mapato kilichokusanywa kilikua ni zaidi kwa Shilingi 13.040 bilioni sawa na asilimia 69.98 Ikilinganishwa na kipindi kama hicho cha Julai - Septemba 2024 ambapo Bandari ilikusanya Shilingi Bilioni 18.631.
Wakati Bandari ya Tanga inaungana na taasisi na makampuni kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, Meneja wa Bandari Bw. Salehe Mbega, amewashukuru na kuwapongeza wadau na wateja kwani wamekuwa sehemu ya mafanikio hayo ya kuvunja rekodi katika utendaji na ongezeko la tija kwa Bandari ya Tanga kwani bila wateja na wadau bandari isingeweza kupata mafanikio hayo.
Bw. Mbega amewahidi wateja na wadau wa bandari kwamba, Bandari ya Tanga imejipanga kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake. "Tukiwa tunaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja sisi kama Bandari ya Tanga tumejipanga kuendelea kutoa huduma iliyobora ya viwango vya Kimataifa ili tuzidi kuvutia wateja wengi zaidi kutumia bandari yetu ambayo imeboresha huduma zake”. Aliongeza Bw. Mbega
Aidha wateja na wadau waliipongeza Bandari ya Tanga kwa kutoa huduma bora kwa wateja wake kwa muda wa saa 24 katika siku 7 za wiki. Wateja hao wamewasihi wafanyakazi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili waendelee kuitumia Bandari ya Tanga.


We celebrate YOU this Customer Service Week 2025! 🌍
#TPA #ports#CustomerServiceWeek #PortsOfProgress
EN
SW
FR


TPA ChatBot - "Nahodha"