Meneja wa Bandari ya Tanga Bw.Salehe Mbega, amewapongeza Wadau wa Bandari ya Tanga kwa ushirikiano katika utoaji wa huduma bora kwa wateja.
Bw. Mbega ametoa pongezi hizo wakati wa Kikao cha Kamati ya Maboresho ya Bandari ya Tanga (Port Improvement Committee - PIC) kilichojumuisha wadau mbalimbali kutoka Sekta binafsi na Taasisi mbalimbali za Serikali.
Katika kikao hicho, kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jengo la Bandari (Bandari House) Jijini Tanga, Bw. Mbega ambaye hicho ni kikao chake cha kwanza tangu ateuliwa kuwa Meneja wa Bandari ya Tanga, alisema kwa sasa shehena imekuwa ikiongezeka kutokana na ushirikiano mkubwa wa wadau wa bandari.
Bw. Mbega ameongeza kuwa wadau ni kiungo muhimu katika maendeleo na ufanisi wa Bandari ya Tanga, hivyo kama kuna changamoto zinazojitokeza ni muhimu kuzitatua kwa pamoja na kwa haraka ili kuendelea kuwavutia wateja kutumia bandari hiyo.
“Sisi sote tunajenga nyumba moja, ambayo ni Bandari hii ya Tanga, hivyo ikifanya vizuri sifa zinakuja kwetu sote lakini pia tukikosea basi lawama zote pia zitakuja kwetu, hivyo ni muhimu kufanya kazi kwa ushirikiano,” amesema Bw. Mbega.


Chama cha Wafanyakazi wa shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA) wa Bandari ya Dar es Salaam wapongezwa kwa kudumisha amani iliyopelekea kuimarika kwa utendaji katika Bandari ya Dar es Salaam.
Akizungumza na wafanyakazi hao wakati akifungua kikao cha 74 cha Baraza la Wafanyakazi la Bandari ya Dar es Salaam mjini Bagamoyo hivi karibuni, Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed Gallus Abed, amewasihi wafanyakazi hao kuongeza ufanisi katika utendaji wao.
“Mwaka uliopita tumefanya vizuri kwa kuwa na tofauti ya tani Milioni nne (4) tu ya lengo tulilojiwekea, mwaka huu tunatarajiwa kufanya vizuri zaidi, hivyo tuwe tayari kufanya kazi kwa ufanisi na ushirikiano pamoja na waendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam ili kutimiza malengo yetu,” amesema Bw. Galus.
Kikao cha Baraza la Wafanyakazi kimelenga kupokea na kujadili utekelezaji wa Bajeti kwa Mwaka 2024/205 na mpango kazi na Bajeti ya mwaka wa fedha 2025/2026.





Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian, ameipongeza Bandari ya Tanga kwa utendaji wenye ufanisi mkubwa katika uhudumiaji wa meli na mizigo ya wateja.
Mhe. Balozi Burian, ametoa pongezi hizo wakati wa ziara yake ya kukagua utendaji wa Bandari ya Tanga.
Katika ziara hiyo Mhe. Balozi Burian alishuhudia meli mbili za mizigo mchanganyiko za MV. Eastern Edelweiss na MV. Zhong Chang Yun 6 zikiwa zinahudumiwa kwa ufanisi mkubwa.
Kwa upande wake, Meneja wa Bandari ya Tanga, Bw. Salehe Mbega alimuhakikishia Mkuu wa Mkoa kwamba, Bandari ya Tanga itaendelea kutoa huduma bora ili kuwavutia wateja wengi zaidi kutumia bandari hiyo.
Aidha pamoja na mafanikio hayo, Bw. Mbega alimuomba Mkuu wa Mkoa asaidie bandari ipate maeneo ya karibu na bandari ili kuiwezesha bandari hiyo kuhudumia shehena kubwa za mizigo mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa alimuhakikishia Meneja wa Bandari kuyapata maeneo hayo ili bandari iweze kuwa kitovu cha shughuli za kiuchumi kwa Mkoa wa Tanga, Taifa pamoja na nchi jirani.
Kwa upande wafanyakazi wa kutwa waliishukuru Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan kwa uwekezaji mkubwa katika Bandari ya Tanga ambao umewezesha watu kupata fursa za ajira nyingi kutokana na kuongezeka kwa meli na shehena.


Bandari ya Dar es Salaam imeandika historia mpya baada ya kupokea meli mpya ya kisasa ya kubeba magari, MV Grande Shanghai, iliyowasili kwa mara ya kwanza ikitokea China katika safari yake ya kwanza.
Meli hiyo iliyokamilika kujengwa Julai 2025 nchini China, ina uwezo wa kubeba magari 9,000, ikiwa na urefu wa mita 220 na upana wa mita 38, ambapo katika safari yake ya kwanza imeshusha magari 1,624 yakiwemo malori, mabasi na magari madogo.
Akizungumza wakati wa mapokezi ya meli hiyo tarehe 21 Septemba 2025, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania( TPA) Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam, Bw. Abed Gallus Abed, amesema ujio wa meli kama hii ni matokeo ya maboresho makubwa yanayofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita pamoja na ushirikishwaji wa sekta binafsi. Alibainisha kuwa uwekezaji katika vifaa vya kisasa umeiwezesha Bandari ya Dar es Salaam kuwa na uwezo wa kuhudumia meli kubwa na za aina yoyote.
Kwa upande wake, Meneja wa Shughuli za Kampuni ya DP World Dar es Salaam, Bw. Elitunu Mallamia, alieleza kuwa ukuaji wa soko na ufanisi wa huduma bandarini ndio vichocheo vikubwa vilivyoleta meli hiyo nchini.
Ujio wa MV Grande Shanghai unaashiria nafasi ya Tanzania kwenye ramani ya biashara ya kimataifa, na unatarajiwa kuongeza mapato ya serikali, kuvutia wawekezaji na kuifanya Dar es Salaam kuwa kitovu cha usafirishaji wa magari na shehena nyingine Afrika Mashariki.


The Tanzania Ports Authority (TPA) Volleyball teams have recorded victories in their recent National League matches. The TPA Men’s team won by 3–0 sets against Moro Warriors, while the TPA Women’s team secured a 3–0 win over Korosho Queens.
These results add to the teams’ consistent performance, with both men and women achieving successive wins in the league. The outcomes reflect the teams’ commitment and discipline as they continue to participate in the ongoing competition.
TPA – Your Gateway to Global Trade and Prosperity.

- KATIBU MKUU WA WIZARA YA UCHUKUZI AFUNGUA KONGAMANO LA KITAIFA LA WADAU WA UCHUMI WA BULUU 2025 JIJINI DAR ES SALAAM
- BARAZA LA MAJADILIANO (CJIC) LA TPA LIMEFANYA KIKAO CHA KAWAIDA JIJINI MOROGORO
- TPA, DP WORLD NA TEAGTL WAENDESHA KAMPENI YA KIMASOKO NCHINI DR CONGO
- TPA KUSHIRIKI KATIKA KONGAMANO LA KITAIFA LA WADAU WA UCHUMI WA BULUU 2025 JIJINI DAR ES SALAAM
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"