Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) Nahodha. Mussa Mandia ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa kuendelea kufanya maboresho katika miundombinu ya kuhudumia shehena katika Bandari zote nchini.

Nahodha. Mandia ametoa kauli hiyo Julai 05,2025 alipotembelea banda la TPA katika viwanja vya Maonesho ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba) yanayoendelea jijini Dar es Salaam.

Viongozi wa Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kwa nyakati tofauti wametembelea Banda la TPA katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ( Sabasaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.

Viongozi hao ni Mkurugenzi wa Masoko na Uhusiano Dkt. George Fasha na Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed Gallus Abed, wameeleza kuridhishwa kwao na elimu ya kuhusu shughuli za kibandari inayotolewa bandani hapo na kuwasihi wananchi kujitokeza kwa wingi.

Banda la TPA katika maonesho ya Sabasaba lipo Katika Kitalu namba 42 Mtaa wa Mataifa ambao pia wapo Waendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Kampuni za DP World na TEAGTL.

Bandari ya Mtwara imeendelea kuhudumia meli kutoka nchi mbalimbali ambapo tarehe 3 Julai 2025 imepokea meli ya MV SEA ARIES kutoka nchini China.

Meli hiyo imebeba tani 5,744.526 za shehena ya mizigo mchanganyiko ikiwemo magari, mitambo na vifaa kazi vya Mradi wa Ujenzi wa Bandari ya Kisiwa Mgao.


Mamia ya Wananchi na Wadau wa Bandari wamejitokeza kwa wingi katika Banda la Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ( Sabasaba) ili kupata elimu kuhusu shughuli mbalimbali za utekelezaji bandarini na kuhusu huduma mbalimbali zitolewazo na Mamlaka.






EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"