Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Albert Chalamila, amemuagiza Katibu Tawala Mkoa wa Dar es Salaam Bw. Abdul Mhinte kuunda timu ya wataalamu kutoka Sekta za Umma na Binafsi katika Mkoa wa Dar es Salaam ili kutafuta suluhu ya kudumu ya msongamano wa malori na magari mengine katika Jiji la Dar es Salaam.

Mhe. Chalamila ametoa maagizo hayo tarehe 11 Julai, 2025 alipokutana na viongozi waandamizi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Wadau wa Sekta za Umma na Binafsi wanaohusika katika sekta ya Uchukuzi na Menejiment ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA).

Aidha, Mhe. Chalamila amewataka Wakala wa Barabara za Vijijini na Mjini (TARURA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kushirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha wanaondoa malori yote yanayoegeshwa kando ya Barabara, hususan barabara zinazoingia na kutoka Bandarini.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) IJP Mstaafu Balozi Ernest Mangu, ametembelea Banda la TPA na kupongeza ushirikiano uliopo kati ya TPA na wawekezaji.

Akiwa kwenye Banda la TPA katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini,Dar es salaam , Balozi Mangu amesema TPA imejipanga kuendelea kuimarisha miundombinu ya Bandari ili kuongeza shehena na ufanisi kwa ujumla.

Kwa kushirikiana na wawekezaji kampuni ya DP World na Tanzania East African Gateway Terminal Limited(TEAGTL) ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam umeimarika kwa kiwango kikubwa na sasa bandari hiyo inaweza kuhudumia meli kubwa.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imefanikiwa kuibuka mshindi wa pili katika tuzo ya Mwezeshaji wa Biashara na Uwekezaji wakati wa Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara yanayoendelea katika Viwanja vya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kupokea tuzo hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TPA, IJP (Mstaafu) Balozi Ernest Mangu amewapongeza Wafanyakazi wa Mamlaka na kuwataka kutumia ushindi huo kama chachu ya kuendelea kutoa huduma bora zaidi kwa wateja.

Naye Naibu Mkurugenzi Mkuu wa TPA Dkt.Baraka Mdima amewapongeza Wafanyakazi kwa ari kubwa waliyonayo katika kutumikia wateja na kuwataka kuzidisha ari ili kuleta tija zaidi

Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Hamis Mwinjuma amewataka Watanzania kutumia ushiriki wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) katika Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa kama fursa ya kuuliza na kupata majibu sahihi ya maswali kuhusu shughuli zote za kibandari.

Mhe.Mwinjuma ametoa kauli hiyo Julai 6 2025, alipotembelea banda namba 42 la TPA lililopo Mtaa wa Mataifa katika viwanja vya Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam.



- MWENYEKITI WA BODI YA WAKURUGENZI TASAC ATEMBELEA BANDA LA TPA KATIKA MAONESHO YA SABASABA
- VINGOZI WA MENEJIMENTI YA TPA WATEMBELEA BANDA KATIKA MAONESHO YA SABASABA
- MV SEA ARIES INAENDELEA KUHUDUMIWA BANDARI YA MTWARA IKIBEBA MITAMBO NA VIFAA VYA MRADI WA UJENZI WA BANDARI YA KISIWA MGAO
- MAMIA WATEMBELE BANDA LA TPA KATIKA MAONEHSO YA SABASABA KUPATA ELIMU KUHUSU SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIBNDARI
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"