Naibu Waziri wa Biashara Jamhuri ya Watu wa China Mhe. Tang Wenhon Aprili 28,2025 amefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam ili kutazama maeneo ambayo nchi yake inakusudia kutoa ushirikiano utakaosaidia ukuaji wa sekta ya Uchukuzi kupitia mpango kazi wa Jukwaa la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).


Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China imeahidi kuendeleza ushirikiano utakaochangia kuimarika na kuukua kwa sekta ya Uchukuzi baina yake na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hususani bandari na reli kupitia mpango kazi wa FOCAC.
Hayo yamejiri katika kikao baina ya Waziri wa Uchukuzi Mhe. Prof. Makame Mbarawa na Naibu Waziri wa Biashara wa China Mhe.Tang Wenhong pamoja na ujumbe wake, makao makuu ya TPA Jijini Dar es Salaam, tarehe 27 Aprili 2025.

Mazungumzo hayo yalilenga kuimarisha ushirikiano kati ya Tanzania na China katika sekta ya usafirishaji na biashara hasa kupitia maboresho ya miundombinu ya bandari, Reli ya TAZARA na Ujenzi wa Reli ya kisasa ya SGR.
Katika mkutano huo, viongozi hao walijadili mikakati ya kuharakisha utiaji saini wa Mikataba ya miradi ya maboresho na ukarabati wa Reli ya TAZARA, kuongeza matumizi ya bandari katika kusafirisha shehena, ambapo Naibu Waziri wa Biashara wa China Mhe. Wenhong, amesisitiza dhamira ya serikali yao kuendelea kuwekeza nchini Tanzania, huku akieleza kuwa maendeleo yaliyofanyika kwenye bandari, Ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR unaoendelea, na ukarabati wa reli ya TAZARA utakaofanyika, vitakuwa kichocheo kikubwa cha biashara na mahusiano ya kiuchumi baina ya nchi hizo mbili.

Kwa upande wake, Waziri wa Uchukuzi wa Tanzania Mhe. Prof. Mbarawa, ameeleza kuwa ushirikiano uliopo baina ya Nchi hizi mbili ni muhimu kwa uchumi wa Taifa na unafungua fursa zaidi kwa wafanyabiashara wa ndani na wa kanda nzima ya Afrika Mashariki.
Mkutano huo umemalizika kwa pande zote mbili kuahidi kuimarisha zaidi urafiki na ushirikiano wa kimaendeleo. Katika Mkutano huo Waziri wa Uchukuzi aliambatana na baadhi ya Viongozi na watumishi kutoka TPA, TAZARA na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

Matukio mbalimbali katika picha wakati Mabalozi wapya wanne, walipofanya ziara ya kikazi Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) ili kujifunza shughuli za utekelezaji Bandarini na kufahamishwa masuala muhimu yatakayowasaidia katika nchi wanazokwenda kuiwakilisha Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, tarehe 25 Aprili 2025.

Mabalozi hao ni Mhe. Balozi Dkt. Habibu Kambanga, aliyepangiwa kwenda nchini Rwanda, Mhe. Balozi Dkt. Suzan Kaganda, aliyepangiwa kuhudumu nchini Zimbabwe, Mhe. Balozi Mobhare Matinyi, aliyepangiwa nchini Sweden na Mhe. Balozi Hamad Hamad, aliyepangiwa kwenda nchini Msumbiji na walipokelewa na kupata maelezo ya kina kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa huduma za Uhandisi Mha. Erick Madinda.

Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), tunaungana na Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuomboleza vifo vya Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), pamoja na dereva wake, Muhajir Mohammed Haule. Tunatoa pole kwa familia, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mheshimiwa Dkt. Doto Biteko, watumishi wa TANESCO, ndugu, jamaa na marafiki.
Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi.
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"