Wafanyakazi Wanawake wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania(TPA) kituo cha Bandari ya Dar es Salaam wameungana na wanawake wote Duniani kuadhimisha siku ya wanawake duniani ambayo kimkoa yamefanyika katika viwanja vya leaders Club vilivyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Maadhimisho hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa Wa Dar es Salaama Mhe. Albert Chalamila yakiwa na kauli mbiu “Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Urawa na Uwezeshaji.
Matukio mbalimbali katika picha wakati Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi Bw. Ludovick Nduhiye, alipotembelea bandari za Mwanza Kaskazini, Kemondo na Bukoba, tarehe 05 na 06 Machi, 2025 kukagua na kujionea utekelezaji wa miradi ya maboresho na upanuzi wa bandari hizo.
Bw. Nduhiye ameipongeza Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) kwa usimamizi makini na ufanisi wa miradi ya upanuzi na uboreshaji wa bandari hizo ambayo ni jitihada za Serikali kupitia Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania ( TPA) katika kuboresha hali ya usafiri na usafirishaji ndani ya Ziwa Viktoria.
Maofisa wa kijeshi kutoka nchini Nigeria wakiongozwa na Air Vice Marshal Titus Z. Dauda wamefanya ziara katika Bandari ya Dar es Salaam kwa lengo la kujifunza masuala ya kiuchumi, siasa na kiutamaduni pamoja na mchango wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA katika maendeleo ya Kiuchumi nchini Tanzania.
Pamoja na Mambo mengine ujumbe uhuo ulipata fursa ya kutembelea kujionea shughuli za bandari ikiwemo gati ya kuhudumia magari 'Roro Terminal " Pamoja na gati 1-7
Ujumbe huo ulipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Bandari ya Dar es Salaam Bw. Abed G. Abed kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu TPA Bw. Plasduce M. Mbossa.
Katika Mitandao ya Kijamii na makundi sogozi, zinasambaa taarifa potofu kwa njia ya sauti kuhusu kuwepo kwa taarifa za uwepo wa Shehena ya Silaha zinazosafirishwa kwenda Kalemie nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kupitia Bandari ya Kigoma. Kufuatia taarifa hizo potofu, Menejimenti ya Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzaia (TPA) inapenda kutoa ufafanuzi kama ifuatavyo


Tanga, Machi 1, 2025
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, amewataka watumishi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) kufanya kazi kwa bidii na uadilifu ili kuongeza ufanisi katika sekta ya bandari, ambayo ni nyenzo muhimu kwa maendeleo ya uchumi wa Taifa.
Mhe. Rais Dkt. Samia ametoa wito huo leo alipofanya ziara katika Bandari ya Tanga kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa gati mbili mpya, unaolenga kuboresha uwezo wa bandari hiyo kushindana kimataifa.
“Bandari ni ushindani. Ni lazima mfanye kazi kwa bidii na kwa uadilifu mkubwa ili tuweze kuongeza ufanisi na kuvutia biashara zaidi,” alisema Mhe. Rais Dkt. Samia.
Ameeleza kuwa maboresho yanayoendelea katika bandari mbalimbali nchini yanahitaji watumishi wa TPA kuwa na ujuzi wa kisasa ili kuendana na mabadiliko ya teknolojia, hivyo amewahimiza kujiendeleza kitaaluma ili kuongeza ufanisi na ushindani katika bandari.
Aidha, Mhe. Rais Dkt. Samia ameagiza Bodi ya Wakurugenzi na Menejimenti ya TPA kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu na haki, akisisitiza kuwa hatavumilia vitendo vyovyote vinavyoweza kuhujumu uchumi kupitia bandari.
“Nimeridhishwa na hatua kubwa ya maboresho yanayoendelea katika bandari zetu, ikiwemo Bandari ya Tanga. Lazima tuhakikishe uwekezaji huu unawanufaisha Watanzania kwa kupunguza gharama za biashara na kuongeza ufanisi wa huduma,” aliongeza.
Akimkaribisha Mhe. Rais, Waziri wa Uchukuzi, Mhe. Prof. Makame Mbarawa, alimpongeza kwa mchango wake mkubwa katika kuimarisha sekta ya bandari, akieleza kuwa uwekezaji unaoendelea umekuwa na matokeo chanya kwa uchumi wa nchi.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Bw. Plasduce Mbossa, alimweleza Mhe. Rais kuhusu hatua za utekelezaji wa mradi wa gati mbili mpya katika Bandari ya Tanga, akibainisha kuwa mradi huo utaongeza ufanisi wa upakuaji na upakiaji wa shehena.
Katika kutambua mchango wake wa kuimarisha sekta ya bandari, Bw. Mbossa alimkabidhi Mhe. Rais Tuzo ya Shukrani kwa uongozi wake thabiti na maelekezo yenye tija katika kuendeleza miundombinu ya bandari na kukuza uchumi wa Taifa.
- KIKAO CHA BARAZA LA MAJADILIANO (JIC) LA TPA KITUO CHA BANDARI YA DAR ES SALAAM
- ZIARA YA WABUNGE KUTOKA BUNGE LA UMOJA WA ULAYA
- MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI JIJINI DODOMA NA MAMLAKA YA USIMAMIZI WA BANDARI TANZANIA (TPA)
- WAZIRI WA UCHUKUZI ARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI WA MRADI MATENKI MAALUM YA KUHIFADHI NA KUSAMBAZA MAFUTA (OIL TERMINAL)
EN
SW
FR
TPA ChatBot - "Nahodha"